Jicho la Mchezaji Latoka Akiwa Anacheza Uwanjani..:;

JANUARY 26: Akil Mitchell       

Mchezaji wa mpira wa kikapu nchini
New Zealand Akil Mitchell amesema anapata nafuu baada ya jicho lake
kutoka alipokuwa uwanjani akicheza.

Mitchell huchezea klabu ya New
Zealand Breakers, na alikuwa mjini Auckland kucheza mechi ya NBL ya
Australia Alhamisi usiku kisa hicho kilipotokea.
Mchezaji wa timu pinzani aliingiza kimakosa kidole ndani ya tundu la kishimo cha jicho na ghafla jicho lake likatoka nje.
Mchezaji
huyo mzaliwa wa Marekani alianguka sakafuni akiwa ametumia mikono yake
kufunika jicho lake la kushoto na akakimbizwa hospitalini.     
“Kwa viganja vya mkono wangu, nilihisi mboni ya jicho ikiwa nje na
kukaa upande mmoja wa uso,” aliambia Radio Sport ya New Zealand.
“Bado jicho hilo lilikuwa linaona.”
“Nakumbuka
nikifikiria, bwana we … hii ni hali mbaya, lakini nilihisi kwamba
lilikuwa jambo la kushangaza na hapo ndipo niliingiwa na wasiwasi
kiasi.”     JANUARI 26: Akil Mitchell Auckland, New Zealand.         JANUARY 26: Akil Mitchell        
Mchezaji huyo wa miaka 24 anasema anakumbuka kusikia mashabiki na wachezaji wake wakiingiwa na wasiwasi.
Alidhani hangeweza kuona tena na kwamba uchezaji wake ulikuwa umefikia kikomo.
“Nilipoingizwa
kwenye gari la kubeba wagonjwa walinipa dawa za kupunguza maumivu na
matoneo kadha ya dawa yenye chumvi machoni na nikasakia mboni ya jicho
ikirudi ndani, jambo ambalo pia lilikuwa la ajabu.”      “Najihisi mwenye furaha sana kuweza kufunga na kufungua macho tena, ni jambo la kushangaza.”                
Baada ya kuruhusiwa kuondoka hospitalini Alhamisi, aliandika kwenye
Twitter kwamba “najihisi vyema” na akatumia picha za vibonzo maarufu
kama emoji za mboni za jicho.
Mchezaji huyo kutoka jimbo la North
Carolina, Marekani anatarajiwa kupona kabisa na huenda akarejea uwanjani
kucheza hivi karibuni. 

COMMENT AND SHARE…………!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2jwGexi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s