Simba Yamnyooshea Yanga Njia ya Kuchukua Ubingwa..:;

Tokeo la picha la simba vs azam 2017           Vinara wa ligi kuu Tanzania bara hivi sasa ni kama inamnyooshea mtani
wake Yanga njia ya ubingwa baada ya leo kukubali kipigo cha bao 1-0
kutoka kwa matajiri wa Jiji la Dar es Salaam, Azam FC, katika dimba la
Taifa Dar es Salaam.                  
Yanga inaweza kukalia kiti cha uongozi endapo itashinda mechi yake ya
kesho ambapo itafikisha pointi 46, ikiwa ni point 1 mbele ya Simba na
hivyo kunogesha zaidi mbio za ubingwa huku Yanga ikiwa kileleni.

Katika mchezo wa leo, alikuwa ni mshambuliaji matata anayefahamika
kwa sifa kuu ya urefu, nguvu na jicho la kuliona goli vizuri, John Bocco
kutoka Azam FC ndiye aliyeibeba timu yake na kuibuka na ushindi huo kwa
bao pekee alilopachika kwa shuti kali katika dakika ya 70.

Bocco amefunga bao hilo baada ya kumzidi uwezo beki wa kutumainiwa wa
Simba, Method Mwanjali baada ya kupigwa ‘kaunta’ moja ya hatari na
Mwanjali kushindwa ‘kukontrol’ mpira ambapo Bocco alikuwa karibu na
kufanikiwa kuunasa na kumtoka Mwanjali, na kuachia shuti upande wa kulia
wa Agyei lililojaa wavuni.

Bao hilo lilifungwa ikiwa ni baada ya Simba kufanya mabadiliko kwa
kuwatoa Jamal Mnyate, Javier Bukungu na Juma Luizio na nafasi zao
kuchukuliwa na Kichuya, Ajibu na Mavugo huku upande wa beki Simba
ikibaki na mabeki watatu kutokana na nafasi ya Bukungu kuwa wazi licha
ya kujaribu kuzibwa na Mzimiru, upande ambao ndiko bao lilikopitia.                        
John Bocco

Licha ya Simba kuzidisha mashambulizi, lakini umahiri wa mlinda
mlango wa Azam Aishi Manula ulizima kabisa ndoto za Simba kuambulia japo
point moja kwa kuokoa michomo kadhaa iliyokuwa dhahiri ikiingia wavuni

Huu unakuwa ni mwendelezo wa Bocco kuzitesa Simba na Yanga na mpaka
sasa anakuwa ndiye mchezaji ambaye ameifunga Simba mabao mengi zaidi
ambapo mpaka sasa ameifunga mabao 19 katika historia ya Simba.

Hiki ni kipigo cha pili mfululizo Simba inapata kutoka kwa Azam baada ya kile cha bao 1-0 katika fainali ya Kombe la Mapinduzi

Kwa matokeo haya Simba bado ipo kileleni mwa ligi ikiwa na pointi 45,
ikifuatiwa na Yanga mwenye pointi 43 ambayo kesho itashuka dimbani
kuvaana na Mwadui FC, na Azam imefikisha pointi 36 ikiwa nafasi ya 4.        

COMMENT AND SHARE……………….!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2k3KB1u

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s