Namna au Jinsi ya Kuzuia Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI..:;

Kondom.jpg              Ni muhimu jamii ielimishwe umuhimu wa kupima afya zao na kuchukua hatua zinazostahili. 

 
Jinsi ya kuzuia maambukizi ya VVU yanayotokana na kujamiiana 
Kutokujamiiana kabisa (kugunga) 
Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu na asiye na uambukizo 
Kujamiiana kwa kutumia kondomu ya kike au ya kiume kwa usahihi na wakati wote 

Jinsi ya kuzuia maambukizi kwa mtoto mchanga 
Wanawake wajawazito wahudhurie kliniki ili kupima na kufahamu  afya zao. 
Washauriwe vilevile wahudhurie na waume au wenzi wao ili  kupata unasihi wa kupima VVU. 
Wanawake wajawazito wanaobainika kuwa na VVU na wenzi wao wa kiume,
wapewe ushauri nasaha (unasihi) kuhusu uamuzi wa kunyonyesha au lishe
mbadala kwa mtoto mchanga
Wanawake wajawazito wanaobainika kuwa na VVU wapewe dawa  za kuzuia
maambukizi kwa mtoto. Familia ambayo mama atakuwa amebainika kuwa na
virusi vya UKIMWI wakati wa ujauzito, ipewe rufaa ili kuendelea na
huduma au matibabu mengine kwa waishio na virusi vya UKIMWI. 
Wanawake wote hasa wale waliobainika kuwa na VVU washauriwe kujifungulia
kwenye vituo vya afya. Wakina mama waliobainika kuwa na VVU ambao
wamejifungulia nyumbani wapeleke watoto kliniki ndani ya masaa 48 baada
ya kujifungua. 
Jamii kwa ujumla ishirikishwe kutoa msaada wa hali na mali kuwawezesha
wakina mama walioambukizwa VVU kutimiza masharti  ya kuzuia mambukizi
kwa mtoto. 
Jinsi ya kuzuia maambukizo ya VVU wakati wa kutoa huduma 
Ni muhimu watoa huduma wawe waangalifu wakati wa kuwahudumiawagonjwa na kuzingatia mambo yafuatayo:
Endapo mtoa huduma ana michubuko, majeraha au vidonda mikononi lazima
vifungwe vizuri kwa kitu kisichopitisha majimaji kama plasta au kuvaa
mipira ya mikononi  wakati wa kumhudumia     mgonjwa Kabla ya kugusa
nguo au vifaa vyenye damu, matapishi, mkojo au kinyesi cha mgonjwa ni
muhimu mtoa huduma kuvaa mipira ya mikononi na mgonjwa aelezwe sababu ya
kufanya hivyo. 
Nguo au vifaa vyenye damu ya mgonjwa au majimaji mengine kutoka kwenye
vidonda viwekwe kwenye maji ya moto yanayochemka kwa dakika 20-30 au
vilowekwe kwenye JIC kwa dakika 20-30 kabla ya kufua/kuosha.  
Mhudumu afue/asafishe vifaa hivyo akiwa amevaa mipira ya mikononi  
Vitambaa vilivyofunga vidonda, mipira ya mkononi ilivyotumika kwa
kumhudumia mgonjwa wa UKIMWI viteketezwe kwa moto.Vifaa vingine
visivyochomeka vitumbukizwe katika choo cha shimo. 
Mhudumu avae mipira ya mikononi wakati wa kumbeba mgonjwa mwenye vidonda. 
Vifaa vyenye ncha kali vilivyotumika wakati kwa kumhudumia mgonjwa wa
UKIMWI na ambavyo vinaweza vikatumika tena vilowekwe kwenye JIC halafu
vichemshwe.  Vile ambavyo havitatumika tena, vitumbukizwe kwenye choo
cha shimo. 
Mhudumu aoshe mikono kwa sabuni kabla na mara baada ya kumhudumia mgonjwa.    
COMMENT AND SHARE……………………….!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2jLTjCS

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s