Je! Morata Atakwenda Arsenal? Kolasinac Ataenda Chelsea na Branislav kwenda Zenit?

Alvaro Morata

Wakati dirisha la uhamisho wa Januari likiwa
linakaribia kufungwa, unadhani ni madili mangapi ya usajili
yatakamilika? Fuatilia Goal kujua zaidi.

Alvaro Morata kwenda Arsenal: 35%


Mshambuliaji huyo wa Kihispania ametajwa kwenye tetesi za kutua Emirates, ikizingatiwa Real Madrid
walikuwa wakitaka kitita cha euro milioni 50 majira ya joto, soko lake
litakuwa linazihusu zaidi timu za Ligi ya Uingereza kwani Paris Saint-Germain tayari wameshamsajili Goncalo Guedes.

Arsenal wamekuwa wakihusishwa na Morata kwa muda mrefu na umri wake wa miaka 24 unambeba katika hilo. Antonio Conte aliyemfundisha Morata akiwa Juventus anaweza akajaribu kumvuta Chelsea.


Sead Kolasinac kwenda Chelsea majira ya joto: 60%


Wakati Juventus wakiwa wanaamini raia huyo wa Bosnia anaweza kuwa mbadala wa muda mrefu wa Patrice Evra,
kiwango cha sasa cha Kwadwo Asamoah kimemfanya uhitaji wake usionekane
tena. Chelsea sasa ndio vinara wa mbio za kumwania, lakini licha ya
uhusiano wao mzuri na Schalke ambako wamempeleka Baba Rahman kwa mkopo,
huenda wakasubiri kumsajili Kolasinac kwa uhamisho wa bure kuelekea
msimu ujao badala ya kutaka kumsajili Januari.


Branislav Ivanovic kwenda Zenit: 55%


Beki huyo mkongwe wa miaka 32 mkataba wake unafika tamati mwisho wa
msimu huu na hajaanza mechi ya Ligi Kuu tangu Septemba; Chelsea imepata
machaguzi mengi katika safu ya ulinzi baada ya kurejea kwa Nathan Ake aliyekuwa kwa mkopo Bournemouth. Zenit wanataka kumsajili Ivanovic kabla ya dirisha la uhamisho wa Januari kufungwa.


Andrea Pinamonti kwenda Liverpool: 15%


Mshambuliaji huyo aliyezaliwa 1999, amekuwa akifuatiliwa na Liverpool
kadhalika Juventus katika mechi alizocheza kwenye kikosi cha vijana wa
Inter na atakuwa na sifa ya kusaini mkataba wake mpya mwezi  Juni
atakapotimiza umri wa miaka 18. Wakati Pinamonti akiwa anafuatiliwa na klabu nyingi, Inter wamedhamiria kumpa mkataba na kumuingiza kwenye timu ya wakubwa msimu ujao.           

COMMENT AND SHARE……………………….!!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2jPJpQt

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s