Mwiguli Nchemba Amkataza DC Makonda Kutembea na Ving’ora vya Polisi..:;

WAKUU wa Mikoa na Wilaya ni ruksa kutembea na magari ya polisi yenye
ving’ora wanapokwenda kwenye shughuli mbalimbali za utendaji, zikiwamo
za ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Ufafanuzi huo ulitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba
wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe
(Chadema) aliyetaka kujua kama ni itifaki za kiserikali kwa wakuu wa
mikoa na wilaya kutembea na magari ya polisi yenye ving’ora.
Mbowe alishangaa na kuhoji kuwa ni itifaki gani kwa viongozi hao, akatoa
mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutembea na kikosi cha polisi chenye
watu tisa, pikipiki za polisi za kuongoza msafara na gari lenye
king’ora.
Waziri Mwigulu alisema, viongozi hao hawaruhusiwi kutembea na misafara
yenye magari ya polisi yenye ving’ora wanapokwenda ofisini, labda kama
viongozi wa mkoa na polisi wapo ofisi moja, lakini hawakatazwi kwenda
navyo wanapoenda eneo la kazi maalumu.
“Viongozi hao wanapokuwa na majukumu ya kwenda kutoa maelekezo au
kufanya shughuli zinazohusiana na majukumu ya ulinzi wa maeneo yao,
wanaruhiswa kuwa na magari hayo,” alisema.  
COMMENT AND SHARE…………………!!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2kofDkO

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s