Tazama Picha za Mtu Aliyeuza Mgongo Wake kwa Mchoraji..:;

Auza mgongo wake kwa mchoraji                   

Tim Steiner ana mchoro mkubwa aina ya tattoo mgongoni mwake.

Alichorwa na msanii mmoja mashuhuri mbelgiji aitwae Wim Delvoye
Na mchoro huo japo uko mgongoni mwake uliuzwa na ukanunuliwa na mkusanyaji sanaa kutoka Ujerumani, Rik Reinking.
Tena,
kuna makubaliano- kwamba Steiner atakuwa akikaa mgongo wazi kwenye
maonyesho akinadi mchoro huo, na hatimae Steiner atakapofariki basi
ngozi yake itatundikwa kwenye fremu kwa ajili ya maonyesho zaidi.
“ndio; Kazi hiyo ya usanii iko mgogoni mwangu, mie nainadi tu ” Steiner mwenye umri wa miaka 40 amenukuliwa akisema.                              Tim Steiner akichorwa          
Steiner mwenyewe aliwahi kufanya kazi kama meneja wa duka la uchoraji
tattoo huko Zurich lakini mpango huo wote ulifanikishwa na rafikie wa
kike ambae ndiye aliyemfahamisha kwa mchoraji huyo wa ubelgiji Wim
Delvoye, aliyekuwa akitafuta mtu ili atekeleze wazo lake hilo tata la
kumchora mtu tatoo mgongo mzima kwa ajili ya kuiuza.
Delvoye alikuwa akifahamika vyema kwa mtindo wake mwengine tata wa kuchora tatoo kwenye migongo ya nguruwe.                                                Nguruwe waliochorwa tatoo                     
Steiner anasema siku mpenziwe alipomwelezea jambo hilo hakusita kamwe -akajibu kwamba yuko tayari.
”mimi
sasa ngozi niliyonayo si yangu, inamilikiwa na Rik Reinking – mgongo
wangu ni kama ‘canvas’ tu ya kuchorea ”anaeleza Steiner kama vile
mzaha!                                             Steiner akiunadi mchoro huo 2012                      
Mchoro huo ulichukua saa 40 kumalizika- na unajumisha vitu vya
kawaida kama maua aina ya waridi na mengineyo , samaki wanaopatikana
sana huko Uchina waitwao koi, picha za watoto, mchoro wa mwanamke
anaefanana na Madona lakini pia mchoro ulio na utata zaidi wa fuvu la
kichwa cha mwanadamu.
Saini ya msanii iko upande wa kulia wa mchoro huo.
‘Kweli ni mchoro mzuri na wa ajabu , mie naupenda ,” Steiner anasisitiza .
Mchoro
huo unaoitwa TIM, uliuziwa mjerumani Rik Reinking hapo 2008 kwa pauni
£130,000 za Uingereza na Steiner akalipwa theluthi moja ya fedha hizo.
“Watu
wengi wanaponiona nimekaa kwenye maonyesho nikiwa nimetulia wanadhani
ni sanamu, kisha wanashangaa sana wakiniona ni binadamu aliye hai.”
Steiner anaendelea kueleza.                                     Mchoro wa tattoo                                
Hata hivyo mchoro huo huzua mijadala mikali , baadhi ya wanaoiona
wakisifia lakini wengine wanafananisha jambo hilo na ukiukaji wa haki za
kibinadamu na hata kuuita utumwa.
Lakini hilo halimbabaishi kamwe Steiner kwani mkataba wake unasema anapaswa kukaa kwenye maonyesho angalau mara 3 kwa mwaka.
Mara ya kwanza alishiriki maonyesho ya Zurich mwezi Juni 2006 .

Lakini mwaka jana wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 10 tangu
tatoo hiyo kuchorwa ilimbidi kuwa katika makavazi kwa kipindi kirefu
zaidi -saa 5 kwa siku kwa situ 6 kila wiki ,kwa mwaka mzima kwenye
makavazi yaitwayo Museum of Old and New Art (Mona) huko Hobart,
Tasmania.                     Steiner akikaa mgongo wazi ili kuunadi mchoro huo                      
Ratiba hiyo ndefu iliisha mwanzoni mwa wiki .
”Ilinibidi
nikae kwenye maonyesho zaidi ya saa 1500 ! Ilikuwa kazi kweli, wakati
mwengine ni kama mwili hauwezi kabisa unataka kujiangusha ulale lakini
nilivumilia na kukaa chonjo kila wakati, hiyo ndio kazi yangu..hayo
ndiyo maisha yangu ! “anasema Steiner.
Japo kuna uzio uliowekwa
watu wasimfikie , wengine wamewahi kuuvuka na kwenda kumgusa , huku
wengine wakipiga mayowe na baadhi hata kumtemea mate.
Hata hivyo hata watu wakimsemea na kumuuliza maswali , yeye huwa hajibu chochote, anakaa tu kimya na kutulia.
Kuna
wakati hata ilibidi Steiner kufanyiwa operation mbili za mgongo
kutokana na maradhi ya mifupa ya mgongo yaliyomkumba kutokana na hali
hiyo ya kukaa kwa vipindi virefu kwenye maonyesho ya sanaa.    

COMMENT AND SHARE…………………………!!!!!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2l5oXJx

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s