Watu Kadhaa Wafariki Wakisubiri Mwisho wa Dunia..:;

        

Waumini watano wanaotambulika chini ya mwamvuli wa imani ya Voodoo
nchini Benin wamefariki dunia baada ya kuamuliwa kukaa kwenye chumba
maalumu na kufanya maombi wakisubiri mwisho wa dunia.
Waumini hao waliamulia kukaa kwenye chumba kilichozibwa sehemu zote kama sehemu ya kudhihirisha imani yao.
Vifo hivyo vilisababishwa na msongamano pamoja na ukosefu wa hewa.
Waumini wengine walionusurika kwenye tukio hilo lililotokea katika Mji
wa Adjarra uliopo karibu na Bandari ya Novo, Kaskazini mashariki mwa
Benin wamelazwa hospitali.
Mmoja wa walionusurika kwenye tukio hilo alisema waliamuliwa kuingia
kwenye chumba cha maombi ili kujisalimisha na adhabu yoyote iwapo dunia
ingefikia mwisho wake.
“Tukiwa katika chumba cha maombi tulitumia nguo zilizochakaa kuziba
maeneo yote yaliyokuwa wazi na baadaye kutayarisha mkaa ambao ulikuwa
kama maandalizi ya kurejea kwa roho mtakatifu,” alisema Yves Aboua akiwa
amelazwa katika hospitali ya Porto Novo.
Tukio hilo linakumbusha lile lililotekea nchini Uganda wakati wafuasi wa
mtu aliyejiita nabii maarufu kwa jina la Kibwetele walipojitekeza kwa
moto wakiamini kuwa mwaka 2000 ulikuwa mwisho wa dunia.
Baada ya tukio hilo iliripotiwa kuwa makumi ya watu walipoteza maisha ndani ya kanisa la Kibwetere.
Kwa muda sasa umekuwapo upinzani mkubwa unaojitokeza kukemea mwenendo
unaofanywa na waumini wa Voodoo ambao wanalalamikiwa kwenda kinyume na
misingi halisi ya imani.
Moja ya kanisa lililojitokeza wazi kukema imani hiyo ni lile linalojulikana kama Kanisa Takatifu la Yesu Kristo wa Baname.
Nchini Benin, Voodoo ni utamaduni unaotambuliwa na wengi na kuna siku
maalumu ya kitaifa inayotambulika kwa jina hilo. Pia, kuna makumbusho ya
Taifa ya Voodoo.         
COMMENT AND SHARE…………………..!!!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2kYAnm4

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s