Mshiriki wa Miss Tanzania Akiri Kudanganya Umri..!!!

         

Aliyekuwa mshiriki wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania mwaka 2008,
Nelly Kamwelu, amekiri kudanganya umri katika mashindano hayo wakati huo
ili apate fursa ya kushiriki mashindano hayo.
Nelly ambaye aliingia katika fainali za Miss Tanzania baada ya kushika
nafasi ya tatu katika Miss Ilala, amesema wakati huo umri wake ulikuwa
ni miaka 15, lakini ilibidi ajikuze ili kukidhi vigezo na kuamua
kuandika umri wa miaka 18.
Nelly amefunguka siri hiyo hivi karibuni akiwa kwenye kipindi cha Friday
Night Live cha EATV ambapo amesema sababu kubwa ya kulazimisha
kushiriki katika mashindano hayo ni ndoto aliyokuwa nayo tangu akiwa
mdogo, lakini pia umbile lake lilikuwa linamruhuruhusu kwa kuwa
alionekana kuwa na mwili mkubwa licha ya kuwa na umri mdogo.
Ukweli huo unaonesha jinsi ambavyo ni rahisi kwa warembo kudanganya umri wao katika mashindano hayo, pasipo kugundulika
Nelly mbali na kushiriki mashindano hayo ya Miss Tanzania ambayo
hakuambulia kitu, anasema hakukata tama na hivyo kuingia katika
mashindano mengine ya urembo ambayo yalikuwa ni Miss Universe Tanzania
mwaka 2011 na kuibuka mshindi.
Hadi sasa anashikilia rekodi ya kuwa mrembo pekee ambaye ameiwakilisha
Tanzania katika mashindano manne tofauti ya dunia ndani ya mwaka mmoja,
kwani katika mwaka huo wa 2011, licha ya kuiwakilisha Tanzania katika
Miss Universe nchini Brazil pia aliiwakilisha Tanzania katika mashindano
ya Miss International mwaka 2011 nchini China na Miss Earth mwaka 2011
Manila, nchini Ufilipino ambapo katika mashindano hayo yote hakufanya
vizuri.
Pia ndani ya mwaka huo huo w 2011 aliiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Miss Tourism Queen International yaliyofanyika Xian, China
na kufanikiwa kukamata nafasi ya 5.   
COMMENT AND SHARE…………..!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2kCmZnh

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s