Kompyuta ya Kampuni ya LG Yashindwa Kufanyakazi na Wi-Fi..:;

Tarakilishi aina ya LG Ultrafine 5K monitor          
LG imekiri kwamba Ultrafine 5K monitor, haiwezi kufanya kazi ikiwa karibu na wi-fi.
Kampuni
kubwa ya uundaji wa vifaa vya kielektroniki LG, imekiri kuwa
tarakilishi yake mpya ya kuonyesha orodha ya bei ya mauzo, “ina matatizo
ya kufanya kazi” hasa inapowekwa karibu na kifaa cha wi-fi.
Screen
hiyo mpya ya LG Ultrafine 5K monitor, inayogharimu kiasi cha Dola 900,
imepigiwa debe pakubwa kama kifaa cha nje cha kuonyeshea orodha ya
bidhaa kwa Mac.
Lakini wateja wamegundua kuwa kuna matatizo katika
maonyesho yake au hata kuzima kabisa inapokuwa karibu na kifaa cha
wi-fi, huku nyingine zikionyesha taarifa potovu katika tovuti ya Apple.
LG imeiambia BBC kuwa wateja wanafaa kubadilisha sehemu ya kuonyeshea bidhaa zao.
“Tarakilishi
hiyo inawasili leo na picha zinatatanika au kuzima na kuwaka inapotumia
Laptopu mpya ya mkononi ya Macbook Pro,” mchunguzi mmoja aliandika.
Mwingine
alioneza kuwa: “kifaa hicho hakijalidwa ipasavyo kutokana na mionzi ya
wi-fi, kwa hivyo inafaa kutoweka kifaa cha wi-fi kama mita mbili karibu
nayo au itazima.
“Kwa hivyo haiko tayari kuuziwa umma.”
Kwa njia ya taarifa, LG imeomba msamaha kwa “kuwatatiza wateja wake” kutokana na kile walichopitia.
“Kubadilisha sehemu au kuweka mbali kidogo kifaa cha Wi-fi, kunafaa kutanzua tatizo hilo”. Imesema.
Kompyuta hiyo mpya ya Ultrafine 5K monitor, imeundwa mwezi huu wa Februari 2017.
Kampuni ya LG sasa inawaomba wateja wake, ikiwa kunaye ambaye atapata matatizo ya namna yoyote, awasiliano nayo.           

COMMENT AND SHARE………………!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2kdTKDV

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s