Man City Yasema Haina Nia ya Kumuuza Sergio Aguero..:;

Sergio Aguero amefungia Manchester City jumla ya mabao 18 msimu huu          
Timu ya Manchester City, haina nia ya kumuuza Sergio Aguero msimu huu
wa kiangazi, licha ya mshambulizi huyo kuachwa nje ya timu katika mechi
mbili zilizopita.
Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 28 alitia
saini kuongeza kandarasi yake msimu huu, ikiwa na maana kuwa anasalia na
miaka mitatu katika mapatano hayo.
Baada ya kutoka benji pale
City ilippopata ushindi wa 2-1 dhidi ya Swansea, Aguero amesema kuwa:
“Bila shaka siondoki, nataka kusalia.
“Katika hili, kwa miezi mitatu ijayo inafaa niisaidie klabu na hapo wataamua kama nina nafasi au la.”
Licha
ya Aguero, kutarajia uamuzi kufanywa msimu huu wa kiangazi, viongozi
wakuu wa Man City, waliashiria siku ya Jumapili kwamba, hawana nia ya
kumuuza mchezaji huyo.
Mchezaji huyo wa mbele wa timu ya
Argentina, alicheza dakika saba za mwisho, pale Manchester City
ilipojipatia ushindi dhidi ya Swansea, baada ya Gabriel Jesus
kujeruhiwa, mechi ya pili kwa mbrazil huyo, aliyechukua mahala pa Aguero
katika kikosi cha kwanza cha wachezaji 11.   

COMMENT AND SHARE……………….!!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2kzjD1U

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s