Mwanasheria wa Wema Sepetu na Vanessa, Albert Msando Afunguka Juu ya Tuhuma Zinazowakabili Wawili Hao..:;

       Mwanasheria wa Wema Sepetu pamoja na Vanessa Mdee, Albert Msando
amefunguka na kuzungumzia nini kinaendelea kwa wateja wake wawili hao
ambao wanakabiliwa na tuhuma za kuhusika na biashara ya Madawa ya
kulevya.

Wawili hao ni miongoni mwa wasanii waliotajwa katika list ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuwa wanatuhumiwa kujihusisha na
biashara ya Madawa ya kulevya.

Wema bado anaendelea kushikiliwa na jeshi lilo huku Vanessa Mdee ambaye
alitajwa katika list ya pili ya RC Makonda na kutakiwa kuripoti kituoni
hapo Jumatatu hii yupo Afrika Kusini na leo amewakilishwa na mwanasheria
wake Albert Msando.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Albert Msando amesema kwa upande wa
Wema bado jeshi la polisi linaendelea na upelelezi na pindi
litakapokamilisha ataeleza nini kinaendelea.

“Mimi nipo hapa kwajili ya Wema Sepetu na Vanessa Mdee,” alisema Albert
Msando. “Kwa Wema bado upelelezi unaendelea, kesho baada ya upelelezi
kukamilika tutajua anapelekwa mahakamani au la,”

Kwa upande wa Vanessa  Mdee mwanasheria huyo alidai muimbaji huyo wa
wimbo Cash Madame bado yupo Afrika Kusini na leo amemwakilisha.

Wasanii wengine ambao bado wanashikiliwa na jeshi hilo ni TID, Nyandu
Tozzy pamoja na Recho na Tunda ambao wamefika leo kituoni hapo.      

COMMENT AND SHARE…………………..!!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2kdB0o4

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s