Serikali Sasa Yajiandaa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi..:;

           
Serikali imesema imejiandaa kukabiliana na changamoto za mabadiliko
ya tabia nchi kwa kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo ujenzi wa kuta
za kuzuia mmonyoko wa ardhi.

Akijibu swali bungeni mjini DODOMA Naibu Waziri wa ofisi ya makamu wa
Rais Muungano na Mazingira, LUHANGA MPINA amebainisha mikakati  hiyo
kuwa ni pamoja na upandaji wa mikoko, kilimo endlevu na ujenzi wa
mabwawa.

Naye Waziri Wa Maji Na Umwagiliaji MHANDISI GERSON LWENGE akijibu
swali la nyongeza amesema serikali inatarajiwa kuweka pampu za kusukumia
maji ili wakazi wanaoishi maeneo yenye mwinuko wilayani BUKOBA waweze
kupata maji safi na salama.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa TAMISEMI, SELEMAN JAFO amesema
serikali itatumia fursa zilizopo kwenye vyanzo vya maji ili kutatua
tatizo la maji lililopo TABORA mjini.       

COMMENT AND SHARE………………!!!!!!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2lhvhyd

Leave a comment