Eric Omondi Amshukuru Sana Diamond Platnumz, Asema Ndiye Aliyemfungulia Mlango Kwenye Soko la Tanzania..:;

                    Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Kenya, Erick Omondi ijumaa iliyopita
ya tarehe 10 alifunguka jinsi Diamond alivyomsaidia kupenya kwenye soko
la Tanzania.

Omondi anasema kwa mara ya kwanza alikutana na Diamond Mombasa nchini
Kenya akiwa kwenye harakati za kurekodi wimbo wa Diamond unaoitwa Nabeba
Mawe.

Katika mazungumzo yao Diamond alimualika Omondi kwenye show kubwa maarufu kama “Zari All White Part” na kumuomba awe MC wa show.

Katika show hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya wahudhuriaji 10,000 , redio
na TV nyingi za Tanzania Omondi hakufanya kosa kama MC, alitumia
kudhihirisha kipaji chake cha uchekeshaji na ikawa ndio mwanzo wa
kujulikana Tanzania.

Omondi anasema bila Diamond kumwalika Tanzania huenda asingeweza kupenya
katika soko la Tanzania, soko lenye mashabiki wengi sana wa kazi zake.

Mpaka sasa Erick Omondi ana mpango katika kipindi cha miezi miwili
ijayo, kuanzisha Comedy TV show nchini Tanzania kwenye moja ya Runinga
maarufu hapa nchini.
Japo hakuweka wazi kipindi hicho kitarushwa hewani kupitia kituo cha habari cha shirika lipi.

Source: NTV ya nchini Kenya.  

COMMENT AND SHARE……………………………..!!!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2lqgFPu

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s