Mkoa wa Mbeya Kinara kwa Matukio ya Kishirikina..!!!

         

MKOA wa Mbeya umetajwa kushika nafasi ya tatu kitaifa, kwa kuwa na
makosa mengi ya jinai na mengi ya makosa hayo, yakitokana na imani za
kishirikina.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele,alibainisha hayo kwenye
mkutano wa Wadau wa Maabara Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, uliokuwa
maalumu kwaajili ya uzinduzi wa kusimikwa kwa mtambo mpya wa Energy
Dispersive X Ray Fluorescence(EDXRF), ambao ni maalumu kwaajili ya
kufanyia uchunguzi wa kimaabara.
Prof Manyele alisema mkoa wa Mbeya, unashika nafasi ya tatu kitaifa kwa
makosa ya jinai, ukiongozwa na mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam. Lakini,
kwa Mbeya hali ni tofauti, kwakuwa matukio mengi yanatokana na imani za
kishirikina.
“Hapa kuna ubakaji hasa wa watoto unaohusishwa imani za kishirikina,
masuala ya mauaji ya kuzika watu wakiwa hai kwa kuwatuhumu kuwa wachawi,
lakini hata biashara nyingi zinazofanyika kwenye mkoa huu zinatajwa
kuhusishwa sana na imani potofu za ushirikina sasa ili kupunguza kiwango
cha makosa ya jinai ni lazima jamii yenyewe ibadilike” alisema.
Akizungumzia mashine ya ED-XRF, Prof Manyele alisema kusimikwa kwa
mtambo huo, kutarahisisha upatikanaji wa majibu ya haraka juu ya
uchunguzi mbalimbali wa kimaabara, ambapo mtambo huo una uwezo wa haraka
wa kuchunguza na kutoa majibu.
Alisema mashine hiyo itatoa fursa kubwa kwa wanajamii, kwa kuwa muundo
wake hautaishia kupimia vinasaba (DNA) tu, bali hata sambuli za madini
ardhini, kemikali zilizopo kwenye vyakula, ardhini na kwenye maji
hususani ya visima virefu na vifupi.
Aliwataka wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, kuitumia mashine hiyo
itakayotoa huduma kwa gharama nafuu, tofauti na zile zilizokuwa
zikigharamiwa kwa sampuli kukusanywa na kusafirishwa hadi Dar es salaam.
Akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Mbeya kwenye mkutano huo, Mkuu wa Wilaya
ya Mbeya, William Ntinika, alisema mtambo huo umekuja wakati muafaka,
ambao Rais John Magufuli amepiga marufuku usafirishaji wa mchanga wenye
madini kwenda nje ya nchi.
 Aliwataka wachimbaji wadogo na wakubwa kuitumia fursa hiyo katika
shughuli zao kwakuwa sasa wataweza kujua sehemu iliyo na kiasi kikubwa
cha madini kwa sampuli za udongo za maeneo husika kupimwa na si kuchimba
kiholela kama inavyofanyika hivi sasa.
Akizungumzia masuala ya Makosa ya jinai yatokanayo na imani za
kishirikina,mkuu huyo wa wilaya alikiri kuwa licha ya uwepo wa makanisa
mengi katika mkoa wa mbeya hata ukalinganishwa na Taifa la Naijeria hali
ya uhalifu ni kubwa ikilinganishwa na mikoa mingine.
“Tulichopanga hivi sasa kama serikali,tumeamua tukutane na viongozi wote
wa dini na wadau wengine ili tukae tuzungumzie suala hili.Ukiangalia
mauaji kila siku,ubakaji kila kona sasa tumeona tukae na hawa wenzetu
ili wanapokuwa kwenye nyumba zao za ibaada wawaambie waumini wao kuwa
Mbeya hatuangaliwi vizuri” alisema Mkuu wa wilaya.
 
 
 
 
 
 
COMMENT AND SHARE…………………………….!!!!!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2mCqRTz

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s