Arsene Wenger: Sijiuzulu Ng’oo, Wanaojiuzulu Huishia Kufa Tu..!!!

Tokeo la picha la wenger                  

Arsene Wenger ametoa mpya na safari hii amesema haondoki kwani wanaostaafu mara nyingi hufa kwa wenye umri kama wake.
Wenger, 67, amekuwa akishutumiwa na mashabiki wa Arsenal kwa kushindwa
kuipa ubingwa na sasa iko nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu ya
England baada ya kufungwa mechi nne kati ya tano ilizocheza.
Kipigo cha mabao 10-2 kutoka kwa Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa
Ulaya, ndicho kilichochochea hasira za mashabiki kutaka aondoke.
Hata hivyo, Wenger ameonyesha hajali na akasema: “Sifikirii kustaafu.
Wanaojiuzulu ni makocha vijana.” Pamoja na kwamba, mkataba wa Wenger
unamalizika mwishoni mwa msimu, lakini Bodi ya Arsenal inampa jeuri
kocha huyo kwani imemwongezea mkataba wa miaka mwili. Alisema pia kuwa
atatangaza hatma yake karibuni.
“Kwa wazee kama mimi, ukistaafu, utakufa,” aliongeza Wenger, muda mfupi
kabla ya mpambano wa jana dhidi ya Manchester City. Wenger anafundisha
Arsenal mwaka wa 21 sasa lakini katika miaka hiyo, hajawahi kuipa
ubingwa katika miaka 13.
“Of course hata mimi inaniuma kukosa mataji,” alisema. “Nikiangalia miaka 20 kwa kweli inaumiza kuona hakuna mafanikio.
“Lakini ukiangalia klabu ya wakati huo na sasa, wakati nilipofika,
wanachama walikuwa saba, lakini sasa kuna watu 700, mambo yanabadilika.”

Alisema: “Ninachukia kufungwa. Ninaelewa kuwa mashabiki wanachukia kila
Arsenal inapofungwa lakini kikubwa ni kushikamana na kila mmoja na kila
shabiki kuangalia timu yetu hadi mwisho wa msimu, hicho ndio cha
kufanya.”     

COMMENT AND SHARE…………………………………!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2nSW0Vr

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s