Bondia Anayefuata Nyayo za Floyd Mayweather Kutetea Taji la Uingereza..:;

Gervonta Davis akisherehekea ushindi katika mojawapo ya mapigano yake         

Bondia anayefuata nyayo za aliyekuwa
bingwa katika uzani wa Middleweight duniani Floyd Mayweather, Gervonta
Davis’ atakuwa ulingoni kuzichapa na Muingereza Liam Walsh – mmoja ya
mabondia watatu kutoka mji wa Norfolk .

Bondia huyo atakuwa wa
kwanza tangu Gervonta Davis kushinda taji lake la IBF huku mechi hiyo
ikitarajiwa kuchezwa katika ukumbi wa Copper Box Arena mjini London.
Gervonta
Davis ni mzaliwa wa Pennsylvania magharibi mwa Baltimore mji ambao
ulikuwa ukikumbwa na mauji siku nenda siku rudi mbali na utamaduni wa
magenge.
Floyd Mayweather ambaye ndio anayemsimamia bondi huyo
kupitia kampuni yake Mayweather Promotion anasema kuwa nduguze Gervinto
walikuwa wakiishi katika chumba kimoja walipokuwa watoto mara nyengine
wakiishi bila chakula.
Gervonta alishinda ubingwa baada ya kumshinda pedrazza kwa njia ya Knockout        
”Nilichukuliwa kutoka kwa mamangu na babaangu nikiwa na umri wa
miaka 4 ama 5 hivi”, alisema Davis anayejulikana kwa jina la utani kama
”Tank’ kwa kuwa na kichwa kikubwa alipokuwa mdogo.
Akiwa na
urefu wa futi 5 na nchi 6, Gervonta Davis anabeba kumbukumbu za kuwaona
wazazi wake wakitumia mihadarati mbali na matatizo ya kuwapoteza
marafiki katika magenge ya Baltimore.
Akiwa na umri wa miaka 22 ameaona shida nyingi.
Lakini
anaingia katika ulingo wa ndondi kutetea taji lake mjini London kama
bingwa akishirikiana na mtu ambaye ameonekana kuwa uso wa ndondi duniani
Floyd Mayweather ambaye anasema kuwa Davis ”ni kama mwanawe”.
Floyd Mayweather anakuza kipaji ambacho amekitaja kuwa bingwa wa ndondi wa siku zijazo.
 Floyd Mayweather akimshauri Gervonta Davis kabla ya pigano          ‘Baada ya kumuona baba na mama wakitumia mihadarati….nimeona mengi
kwa hivyo hakuna kitu ambacho mtu mwengine anaweza kufanya ili
kuniumiza”.
Uchungu mwingi na makovu ya ujana yalimwacha Davis kuwa bondia mzuri ambaye alikuwa amekosa muongozo.
Alipendelea
sana masomo akiwa shule, lakini wakati mjombake alipomuona akipigana
mtaani alimchukua na kumpeleka katika jumba la mazoezi ya ndondi ili
kuanza maisha mapya.
Calvin Ford ambaye alipigana ndondi kwa miaka
10 akiwa jela anasema kuwa yeye na Davis walisaidiana sana wakati
maisha nyumbani yalipokuwa mabaya na kumfanya Davis kuishi kwa bibi
yake, jumba hilo la mazoezi lilimsaidia kushinda mataji ya kitaifa na
kuonja utamu wa ndondi. 
           ”Hivi sasa ningekuwa jela ama hata marehemu lakini niliamua kukaa
katika jumba la mazoezi na miaka kadhaa baadaye nimesajiliwa na bondia
maarufu zaidi duniani”, alisema Davis.    

COMMENT AND SHARE……………..!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2q66b7A

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s