Hatima ya Meneja wa Arsenal(Arsene Wenger) Kuamuliwa.:;

Arsene Wenger                

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
amesema hatima yake katika klabu hiyo itaamuliwa katika mkutano wa bodi
ya klabu hiyo baada ya fainali ya Kombe la FA mnamo 27 Mei.

Mfaransa huyo wa miaka 67 amekuwa na Gunners tangu 1996 na mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwisho wa msimu huu.
Wenger
amekuwa akishutumiwa sana na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo, na
kunao ambao wamekuwa wakiweka mabango kumtaka ajiuzulu.
“Kuna mambo mengi ambayo yatajadiliwa katika mkutano wa bodi. Moja, ni nini kitamtendekea meneja,” amesema. 
“Bila shaka nitakuwepo. Kwa sasa tunafaa kuangazia yaliyopo sasa na
ni kwamba tunacheza Jumapili na tuna fainali ya Kombe la FA.”
Klabu
hiyo ya London kaskazini itakutana na mabingwa wa ligi Chelsea
uwanjani Wembley, tumaini pekee la Arsenal kushinda kikombe msimu huu. 
Arsene Wenger banner                 
Arsenal wamesalia kucheza mechi moja pekee ligini, ambapo wana
kibarua cha kujaribu kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwani wamo
nafasi ya tano, alama moja nyuma ya Liverpool walio nafasi ya nne na
tatu nyuma ya Manchester City, lakini wanapungukiwa na mabao.
Arsenal
watakuwa wenyeji wa Everton mechi ya mwisho Jumapili (15:00 GMT), nao
Liverpool watakuwa wenyeji wa Middlesbrough uwanjani Anfield nao
Manchester City wasafiri Watford. 
Wenger aliongeza: “Lazima tufanye kazi yetu, sisi ni wataalamu na
tunataka kushinda. Tumekuwa katika mbio nzuri na tunachoweza kufanya kwa
sasa ni kushinda mechi yetu ya Jumapili. Baada ya hapo,
kitakachotendeka kunihusu si muhimu.”
“Niko hapa kuitumikia klabu na njia bora zaidi ya kufanya hivyo ni kushinda mechi ijayo.” 

COMMENT AND SHARE………………………….!!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2pYRAib

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s