Msani Riyama Alia na Umaskini wa Bongo Movies..:;

          Msanii wa bongo movie Riyama Ally amefunguka na kusema licha ya kufanya
kazi ya filamu kwa miaka zaidi ya 15 lakini hajapata mafanikio yale
ambayo watu wanategemea angekuwa nayo kutokana na uwezo wake wa kuigiza.

Rihaya Ally alisema hayo jana alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night
Live na kusema hakuna kitu kinaumiza kama unapofanya biashara na kulipa
kodi halafu mshindani wako ambaye anafanya biashara hiyo hiyo anafanya
mambo kinyume halipi kodi, kazi yake ni kufyatua tu filamu na kuziingiza
sokoni.

“Kikawaida changamoto katika biashara ni nyingi na hakuna biashara
ambayo haina leseni au haulipi kodi, na kikawaida kila jambo linafanyika
katika misingi ya sheria hatuwezi kufanya kitu kinyume cha sheria, kwa
hiyo sisi tunalipa kodi halafu wenzetu inakuwa tu wanafyatua filamu bila
kulipa kodi, hiyo inaumiza sana sababu mimi nipo kwenye game kwa zaidi
ya miaka 15 sina baiskeli, sina bajaji, sina gari sina chochote”
 alisema Riyama Ally

Mbali na hilo Riyama Ally anasema wasanii wengi wanashindwa kufanikiwa
kutokana na mambo kama hayo, ila anawataka wasanii wa bongo kujipanga na
kutengeneza filamu ambazo wananchi wanazihitaji na kusema kuzuia filamu
za nje zisiingie ni jambo la ajabu

“Kutokana na mambo hayo hayo wasanii wengi wanashinda kufanikiwa lakini
kama wenzetu wangekuwa wanalipa kodi kama sisi basi hakuna tatizo, kama
ukiwa msanii mzuri na unakidhi mahitaji ya jamii huwezi kuhofia kazi za
nje maana hizo ndiyo kioo chetu sisi, wenzetu wametutangulia sana
inabidi tujifunze kupitia wao, kwa hiyo zinatakiwa kuendelea kuingia
lakini kwa kufuata utaratibu ili na kazi zao nao zilipiwe kodi nchini”
alisisitiza Riyama.  

COMMENT AND SHARE………………………..!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2rFH0sH

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s