HESLB Yavuka Lengo, yakusanya Kiasi cha Shilingi Bilioni 116.:;

       
 Zoezi la utafutaji, ufuatiliaji na ukaguzi wa wadaiwa sugu na ambao
wamenufaika na mikopo ya elimu ya juu mahala pa kazi iliyoendeshwa na
Bodi ya Mikopo ya Mikopo ya Elimu ya Juu katika kipindi cha mwaka mmoja,
limefanikiwa kwa asilimia 46

na kupelekea makusanyo ya mikopo hiyo kuvuka lengo lililokusudiwa.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, kuhusiana na
hali ya makusanyo ya mikopo kwa wanufaika wa elimu ya juu, Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bwana Abdulrazak Badru
amesema walilenga kukusanya Shilingi Bilioni 76 lakini wamekusanya
Shilingi Bilioni 116 ikiwa ni kiwango cha marejesho cha asilimia 46.

Bwana Badru amesema, hataacha kutumia mbinu ya ufuatiliaji mahala pa
kazi huku akiwakumbusha wale ambao wanashindwa kurejesha mikopo kwa
hiari sheria itafuata mkondo dhidi yao kwani fedha hizo hutumika kwa
wanafunzi wa awamu mpya ya masomo.

Aidha, Bwana Badru ametoa onyo kali kwa waajiri ambao wameshindwa
kuwasilisha majina ya waajiriwa wao ndani ya siku 28 kwa bodi hiyo,
kuchelewesha makato baada ya kuwakata waajiriwa ama kuficha taarifa kuwa
hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

COMMENT AND SHARE………………………!!!!!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2tJheb8

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s