Huu Ndio Utajiri Mkubwa Utakaoupata, Kama Utaamua Mwenyewe Kufanya Biashara Hii..:;

        
MAKALA HII IMEANDIKWA NA MESHACK MAGANGA WA IRINGA TANZANIA.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitoa hamasa kwa vijana wenzangu wa kike na
kiume na watu wa kada mbalimbali, wito wangu umekuwa nikuwataka vijana
wenzangu kauanza utamaduni wa kuwekeza kwa muda mrefu na kujifunza
ujasiriamali. Ninaandika makala hii kutoa ushuhuda wa niliyoyafanya kwa
muda wa zaidi ya miaka miwili iliyopita na kuniletea mafanikio makubwa.

Nilianza kujishighulisha na ujasiriamali nilipokuwa chuo kikuu mwaka wa
pili, kwa kuuza vocha na  kazi ya ‘steshenari’ na uuzaji wa laptop,
sikuendelea nazo sana kwa sababu ya kubanwa na masomo yachuo.
Nilipomaliza chuo 2010, nilianza kilimo cha mboga na kufuga kuku hapa
Iringa mjini, baada ya hapo kaka yangu alianza kunihimiza kuhusu kilimo
cha miti ambacho yeye mwenyewe anafanya.

Na baadaye nikakutana na rafiki yangu Albert Sanga ambaye pia
anajishughulisha sana na kilimo cha miti. Tangu 2011 nilinunua shamba la
ekari 10 na kuzipanda miti hela ambayo niliipata baada ya kuuza matango
niliyolima kijijini Kalenga, nikaongeza bidii zaidi ya kulima matango
na kununua mashamba, leo nina ekari nyingi.

Albert sanga, mjasirimali na mwekezaji alipata kuandika haya kuhusu
mimi:- “UNASUBIRI UPATE MTAJI? OPSss! UNAWEZA KUFA MASIKINI! Nina rafiki
yangu mpambanaji kweli kweli na msomi wa chuo kikuu wa mambo ya
maendeleo na elimu; na mtaalamu wa IT, anaitwa Meshack Maganga. Wakati
fulani huko nyuma alinifuata na kuniambia, “Sanga nimeamua kuanza
kui-invest katika mashamba ya miti; mtaji wa kuanzia nina tsh elfu
ishirini na tano, (25,000?/=).

Nikamwambia “Kupata ekari moja si chini ya laki sita na wewe una tsh
25,000/= utawezaje?” Akanijibu “Nitaweza!”, Sikumwelewa! Kumbe alikuwa
anaona mbali! Alichofanya alichukua hiyo 25,000/= akaenda nayo eneo moja
linaitwa Kalenga (km 20 kutoka Iringa mjini) huko akalima matango.
Angalia mchanganuo: Shamba nusu eka akakodi kwa tsh 10,000/=, mbegu za
matango akanunua Tsh. 7,000/=.

Kwenye kulima akalima kwa mikono yake akisaidiana na kibarua mmoja.
Fedha iliyobaki 8,000/= akalipa kibarua na kununulia dawa ya kuua
wadudu. Alipokuja kuvuna akapata tsh 800,000/= (laki nane). Alipokuja na
fedha hii tukaenda kutafuta shamba la miti akaanza na ekari moja huku
pesa nyingine akairudisha shambani.

 
Hivi leo Bw. Maganga ana ekari zisizopungua hamsini za mashamba ya miti
na anaendelea na kilimo cha umwagiliaji. Lakini HAPO amefika kwa kutumia
tsh 25,000/= tu. Tunaposema hauhitaji mamilioni kujiajiri tunatamani
ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa kama Bw. Maganga. Unaweza kumwandikia”
Akaendelea kwa kusema:-

Kuhusu kilimo cha miti ninacho kifanya mimi na nimepania kwelikweli
ndani ya nchi yangu niipendayo Tanzania ni kwamba, kimepata umaarufu wa
ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo
ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya mazingira. Katika
Tanzania mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu
mikubwa ya kupandwa.

Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea pamoja na
utengenezeaji wa karatasi. Ukiacha mahitaji haya tuliyoyazoea; hivi sasa
kumeibuka fursa nyingine mpya ambapo mashirika ya kimazingira kutoka
Magharibi yananunua hewa ukaa. Kwa maana hiyo unaweza kupanda shamba la
miti halafu ukawa unakusanya dola kwa kuuza hewa ukaa wakati ukisubiri
miti ikomae uvune mbao, nguzo ama miti ghafi ya kutengenezea karatasi.

Hii ni sawa na kutegeneza hela ukiwa umelala. Mbali na kuuza hewa ukaa,
vile vile unaweza kufuga nyuki na kuendelea kuvuna asali wakati
unasubiri kukusanya mamilioni kwa kuuza miti ya nguzo, karatasi ama
mbao.Kilimo hiki cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu
(middle& long term investments). Kiutamaduni watanzania wengi huwa
hawavutiwi na uwekezaji wa muda mrefu.

 
Hata hivyo kama una mpango wa kuwa na “financial freedom” usikwepe
kufikiria uwekezaji wa muda mrefu. Waingereza husema “Information is
power”. Wengi hawajachangamkia fursa hii kwa kukosa taarifa tu. Kazi
yangu leo ni kukupa taarifa hizi za utajirisho. Miti ya mbao inatumia
wastani wa miaka sita hadi 8 au saba, tangu kupandwa hadi kuvunwa kwake.

 Hii ina maana inapofikisha umri wa miaka sita huwa tayari kwa kuanza
kuvunwa kwa mbao ndogo. Ekari moja ya shamba inachukua wastani wa miti
mia sita (600). Wastani wa chini wa mti mmoja kwa sasa uliokomaa ni
shilingi elfu ishirini (30,000 hadi 60,000,inategemea na ukubwa wa mti).
Ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa unakusanya jumla
ya shilingi milioni kumi na nane (18,000,000).

Fedha hiyo (kadirio la chini kabisa) utaipata ikiwa unaamua kuuza kwa
bei ya jumla miti ikiwa shambani. Lakini kama ukiamua kupasua mbao wewe
mwenyewe unaweza kuvuna mbao hadi za milioni thelathini na mbili
(32,000,000) kwa ekari moja. Hadi sasa uhitaji (demand) wa mbao katika
soko ni mkubwa kuliko ugavi (supply) hivyo kwa miaka 10 ijayo
hatutarajii kushuka kwa soko la mbao, nguzo ama malighafi za karatasi.

Gharama ya kununua shamba tupu ni kati ya shilingi  laki moja na 20 elfu
(120,000) na laki moja, kutegemea na maeneo husika unayotaka ama
kupata. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni kati ya
shilingi laki moja  na nusu,na laki moja. Hii ina maana unaweza kumiliki
ekari moja ya msitu wa miti kwa hadi shilingi laki sita tu! Kutegemea
na umri wa miti unayotaka.

Mtu unaweza kuona kuwa pengine kununua shamba tupu na kuanza kuhangaika
na upandaji miti itakuwa ni mlolongo mkubwa; kukusaidia katika hilo
nimekuwa na utaratibu wa kumilikisha mashamba yenye miti (kuuza) kwa bei
nafuu sana. Yapo mashamba yenye miti ya kuanzia mwaka mmoja, miaka
miwili, miaka mitatu na miaka minne.

 
Uponunua mashamba haya kutoka kwangu, mimi naendelea na upandaji wa
mashamba mapya kupitia fedha hizo. Kilimo cha miti ni rahisi sana kwa
sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi mkubwa sana na wala hauhitajiki
uwe karibu na shamba/mradi muda wote. Kuna kazi chache ambazo
zinahitajika ukishapanda shamba lako.

 
Mvua inyeshe ama isinyeshe mti wa mbao, nguzo ama karatasi ukishachipua
huwa haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini. Kazi namba moja
unapokuwa umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba; ni kutengeneza
njia za kuzuia moto walau mara moja kwa mwaka, kazi ya pili ni kufyekea
miti inapokua walau kwa mwaka mara moja (prooning).

 
Gharama zote hizo yaani kutengeneza njia za moto, kufyekea na kulinda
moto haizidi laki mbili kwa mwaka mzima. Kwa maana hii gharama za
kuhudumia shamba la miti ekari moja kutoka kupandwa hadi kuvunwa ni
wastani wa shilingi milioni moja tu. Gharama hizi ninazopiga ni ikiwa
utaamua kununua shamba leo na kama ungekuwa tayari una shamba ambalo
unalihudumia leo.

 
Hata hivyo nadhani wote tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda
thamani kila siku. Vile vile tunatambua kuwa suala la mazingira ni tete
kwa sasa na katika karne zijazo kama wataalamu wanavyotuthibitishia. Hii
ina maana kuwa ukiwa na shamba la miti leo; thamani ya ardhi hiyo
inazidi kupanda kila siku na miti uliyopanda inazidi kupanda thamani
kila kukicha.

 
Jambo la uhakika ni kuwa hata kama bei ya miti, mbao, nguzo itayumba
hutaweza kupoteza mtaji uliotumia na wala hutakosa kuzalisha faida kwa
shamba utakalokuwa umemiliki, iwe ni eka moja, kumi, mia ama elfu moja.
Mbali na hivyo unaweza ukaona, ahaa, miaka sita hadi kumi ni mingi mno;
bado una nafasi ya kupata faida hata ndani ya mwaka mmoja, miwili au
mitatu.

 
Ukishapanda shamba la miti ekari moja kisha baada ya mwaka mmoja ukaamua
uuze utauza si chini ya milioni mbili hadi nne. Kukusanya milioni nne
kwa mtaji wa laki sita, pasipo kutumia muda mwingi ama usumbufu wa
kusimamia; hakika ni faida nono.

 
Huenda hadi kufika hapa unaweza ukawa umeshavutiwa na biashara hii.
Wengi wenu mnaweza kujiuliza maswali mkubwa mawili; “Ninatamani nifanye
mradi huu lakini Iringa sikufahamu na hata kama nakufahamu nitaanzia
wapi kupata hayo maeneo?” Pili: Niko mbali na sina muda wa kushinda
Iringa, Je, ni nani atanisaidia kupanda, kusimamia na kuendesha hayo
mashamba?

 
Ili kutimiza ndoto yangu hiyo nimeweka utaratibu ufuatao utakaohakikisha
kila mwenye ndoto, kiu na hamasiko la kuwekeza kwenye kilimo cha miti
anafanikiwa.  Jisikie huru wakati wowote kuwasiliana nami kwa ufafanuzi
na msaada wa fursa hii. Natamani watanzania tuache kulalamika kuhusu
wageni kuvamia ardhi yetu, badala yake tuchangamke kumiliki na kufanya
uzalishaji katika ardhi yetu.

 
Inawezekana! Kwa kutumia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 sheria namba 5
utapata documents za umiliki; kwa kuzingatia taratibu na tamaduni zote
za wenyeji zinazohusiana na umilikaji ardhi nitahakikisha nakusaidia ili
ndoto yako itimie.

 
Yupo Baba yangu anaishi Mafinga ambae siku za karibuni amepewa Tuzo ya
Rais kwa kuwa mpandaji namba moja wa miti na utunzaji wa mazingira,
ameahidi kutoa msaada kwa Mtanzania wa ndani na nje ya Tanzania kumsadia
kupata eneo la kupanda miti na kauli ya siku zote ni “USIKUBALI KUWA
MNYONGE WA KIUCHUMI NDANI YA TANZANIA.

COMMENT AND SHARE……..!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2tJD3r1

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s