Mayweather na McGregor nusura wazichape kavukavu .:;

       
Rais wa UFC, Dana White (katikati) akijaribu kuwatenganisha Floyd
Mayweather (kushoto) na Conor McGregor wasipigane ‘kavu kavu’ usiku wa
jana ukumbi wa LA’s Staples Center mjini Los Angeles, Marekani  
 
MPIGANAJI Conor McGregor ametamba kummaliza katika raundi ya nne bingwa
wa dunia wa ngumi za kulipwa ambaye hajawahi kupoteza pambano, Floyd
Mayweather katika ufunguzi wa ziara ya promosheni ya pambano lao la
Agost 26, mwaka huu mjini Los Angeles, Marekani.
 
Mbele ya mashabiki 11,000 ukumbi wa LA’s Staples Center, Mayweather na
McGregor walikutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza tangu kuthibitishwa
kwa pambano lao la utajiri mkubwa.

 
Licha ya kutokea mbele ya umati wa mashabiki wa nyumbani na kuvaa
tracksuti yenye rangi za bendera ya Marekani, lakini Mayweather
alijikiuta akizomewa huku mpinzani wake kutoka Ireland, McGregor
akishangiliwa kila alipotokea kwenye kioo kikubwa chaTelevisheni.

 
“Atazimika ndani ya raundi nne. Hana uzoefu wa hii. Simuogopi. Huu ni
mchezo wenye sheria zinazokubana na kulifanya hili liwe nusu pambano.
Kama hili lingekuwa pambano, asingemaliza raundi hata moja,”alisema
McGregor akimaanisha wangepigana katika mchezo wake wa UFC wa
kuchanganya na mateke angemmaliza mapema zaidi Mayweather.

 
Lakini ‘bishoo’ Mayweather naye hakuwa kimya, kwani alijibu tambo za
mpiganaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anayejiandaa kwa pambano la
kwanza kabisa la ngumi bila mateke kiasi cha wawili hao kukaribia
kupigana ‘kavu kavu’.

 
“Ni bwana mdogo, yupo katika miaka ya 20, nipo katika miaka ya 40. Damu
yake inacheka, siyo mimi” alisema Mayweather ambaye pia alidai pambano
hilo lina mvuto mkubwa wa kishabiki.

 
“Nimekuwa nikifanya hivi kwa miaka 20. Nimekuwa hapa kabla. Lakini ni
mgumu. Ni shujaa. Bora lazima apigane na bora. Mashabiki wamelitaka
pambano hili, McGregor amelitaka pambano hili, nimelitaka hili pambano.
Agost 26 itakuwa machozi, jasho na damu tangu kengele ya ufunguzi,”
amesema.

COMMENT AND SHARE………………………!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2tJd82R

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s