Wachezaji wa Everton watua Dar es Salaam Tanzania tayari kukabili Gor Mahia.:;

Rooney na wachezaji wa Everton      

Wachezaji wa klabu ya Everton kutoka
England wamewasili jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa ziara yao
ya kwanza kabisa Afrika Mashariki.

Wachezaji hao na wakufunzi pamoja na maafisa wengine wa timu walifika uwanja wa ndege saa mbili asubuhi kutoka Liverpool.
Ziara yao ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi ya Premia.
Miongoni
mwa wachezaji waliosafiri Tanzania ni Wayne Rooney ambaye amerejea
katika klabu hiyo bila kulipiwa ada yoyote baada ya kukaa miaka 13 klabu
ya Manchester United.    
Wachezaji wa Everton      
Mashabiki wengi wa soka ya England wamesafiri Tanzania kushuhudia
Everton wakichuana na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia katika uwanja wa
taifa wa michezo jijini Dar es Salaam.
Uwanja huo una uwezo wa kutoshea mashabiki 60,000.
Rooney anatarajiwa kucheza katika mechi hiyo ya Alhamisi.
Wengi
wa mashabiki waliofika nje ya hoteli wanamokaa Everton jijini Dar es
Salaam waliimba “Rooney Rooney” mchezaji huyo aliposhuka kutoka kwenye
basi kuingia hotelini.
Kulikuwa pia na kundi la raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao walijawa na furaha kumuona mwenzao Yannick Bolasie.
Wachezaji wa Everton     Wachezaji ngoma wa Kimaasai waliofika kuwatumbuiza wachezaji hao    
Wachezaji wa Everton
Waliimba nyimbo za kitamaduni za DR Congo naye Bolasie akawajibu kwa kucheza.
Mechi ya kesho imeandaliwa na kampuni ya SportPesa kusherehekea udhamini wa jezi za klabu ya Everton.
Wakati
wa ziara yao, wachezaji wa Everton pia wataandaa vikao vya mafunzo ya
soka na kucheza pia dhidi ya timu mseto ya wachezaji wenye matatizo ya
ngozi, Albino United, kuhamasisha watu kuhusu mashambulio na dhuluma
ambazo zimekuwa zikitendewa watu wenye ulemavu huo.
Wengi wamekuwa wakiuawa Tanzania na nchi jirani kwa sababu ya ushirikina.
Wachezaji hao baadaye wameelekea shule ya watoto wenye ulemavu ya Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es Salaam.
Shule hiyo hupokea ufadhili kutoka kwa shirika la kutoa msaada nchi za nje la Uingereza, DFID.
Baadaye, wachezaji hao wanatarajiwa kucheza na watoto hao.  
Wachezaji wa Everton wakiwa shule ya Uhuru Mchanganyiko    

COMMENT AND SHARE…………!!!!!!!!

via Blogger http://ift.tt/2u9NO6Y

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s